WICOM LIWALE WAALIKWA SIKU YA SHERIA TANZANIA

Kushoto ni hakimu mfawidhi liwale Hon.Charles Makwaya na katikati ni mkuu wa wilaya wa Liwale Hon.Goodluck Mlinga na kulia ni DAC Liwale Hon.Azilongwa Bohari na nyuma katikati ni meneja wa WICOM tawi la Liwale ndg.Majaliwa Mgagani akiambatana na meneja wa nmb na crdb

Jukwaa liliwakutanisha wanufaika wa huduma mbalimbali za kimahakama katika kusherehekea kilele cha siku ya sheria ambayo kila mwaka hufanyika tarehe 02/02/2026

Katika sherehe hizo WICOM tawi la Liwale iliwakilishwa na meneja wa tawi hilo Ndugu. Majaliwa Mgagani ambaye pamoja na mengine mengi aliwasilisha ujumbe wa kampuni ya WICOM katika sherehe hizo ambao ni ahadi ya kuendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kimahakama kwa mujibu wa sheria za nchi.

WICOM kama ilivyo ada kwa siku zote, itaendelea kushirikiana na serikali na katika kutekeleza majukumu mbalimbali kwa maendeleo ya taifa.

Related Posts

Wicom Support

Typically replies within a day