HADITHI YA MAFANIKIO YA ‘SUPER IMRAN’MJASIRIAMALI ALIYE KUZA BIASHARA YAKE KUPITIA WICOM FINANCE

Mtwara, Tanzania

Katika kuendeleza adhima yetu ya kusaidia jamii na kukuza biashara ndogo hapa nchini, taasisi ya fedha ya WICOM FINANCE imeendelea kuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyabiashara . Hivi karibuni, taasisi imetembelea na kujionea mafanikio makubwa ya mteja wake, Bwana Hassan Idd Matata, mwenye umri wa miaka 37 anayeendesha duka maarufu la vyakula na nafaka linalojulikana kama “SUPER IMRAN” lililopo mkoani Mtwara. Kupitia ushirikiano huu, WICOM FINANCE inathibitisha kwa vitendo kaulimbiu yake ya “Together tunasonga mbele“.

Kabla ya kupata huduma za kifedha kutoka WICOM FINANCE, biashara ya Bwana Hassan ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya mtaji mdogo uliosababisha duka lake kukosa baadhi ya bidhaa muhimu na kupunguza kasi ya ukuaji wake. Hata hivyo, baada ya kupatiwa mkopo wa kibiashara wa Shilingi Milioni Tano kwa muda wa miezi mitatu, mambo yalibadilika kwa haraka. Mtaji huo ulimuwezesha kuongeza shehena ya kutosha ya vyakula na nafaka dukani kwake, jambo lililoongeza mzunguko wa wateja na kukuza kipato chake kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza kwa furaha wakati wa mahojiano hayo, Bwana Hassan Idd Matata ameishukuru sana taasisi hiyo kwa kusema kuwa mkopo huo umemsaidia kwa kiwango kikubwa kupanua wigo wa biashara yake na hata kufungua biashara nyingine mpya. Kwa sasa, mjasiriamali huyu ana malengo makubwa ya kuendelea kutanua wigo wa biashara yake katika maeneo mengine zaidi. WICOM FINANCE inajivunia kuwa sehemu ya mafanikio haya na inawakaribisha wafanyabiashara wote nchini kujiunga nayo ili kukuza mitaji na kutimiza ndoto zao za kibiashara.

Related Posts

Wicom Support

Typically replies within a day