
Ashura Abilah Namchochi(Bibi Nihani) ni mjasiriamali shupavu wa miaka 43 kutoka Masasi Mtwara, alikuwa akipambana kuendesha duka lake la bidhaa mchanganyiko katika mazingira magumu. Kwa muda wa mwaka mmoja, alikumbana na changamoto ya ukosefu wa bidhaa za kutosheleza mahitaji ya wateja wake, hali iliyofanya biashara yake kuwa dhaifu na kusuasua. Alihitaji msukumo wa ziada ili kuweza kutoa huduma bora na kukuza duka lake ambalo ni tegemeo lake la kila siku.

Mabadiliko yalianza pale Ashura alipoamua kuchukua mkopo wa “INUKA” wa thamani ya Tsh 400,000 kutoka WICOM Finance. Ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu, alitumia mtaji huo kuongeza bidhaa na kuboresha duka lake kwa kiasi kikubwa. Leo hii, duka lake lina muonekano mpya na wa kuvutia, likiwa na shehena ya kutosha ya bidhaa kuanzia vinywaji, vyakula, hadi mahitaji madogo ya nyumbani, jambo ambalo limemfanya mteja huyu kuwa na furaha na amani katika biashara yake.

Matunda ya uwekezaji huu yameonekana wazi; kipato chake kimeongezeka na sasa ameweza hata kufanya maboresho makubwa nyumbani kwake na kuanza kuweka akiba kwa ajili ya kesho. Ashura anajivunia kuwa na mtaji imara na ana mpango wa kuendelea kuikuza biashara yake iwe kubwa zaidi ili kufikia mafanikio makubwa ya kimaisha. “Biashara imekuwa na mtaji upo vizuri,” anasema Ashura akionyesha tabasamu la ushindi. Tunajivunia kuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya wajasiriamali kama yeye! Huu ni uthibitisho tosha kuwa uwezeshaji mdogo unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jamii yetu.
