
Kupitia mwaliko rasmi wa Ruangwa Queens Club, kampuni yetu ilishiriki katika kutoa msaada wa maji
safi kwa timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.
Katika tukio hili, kampuni iligawa katoni za maji safi kama sehemu ya mchango wake katika kuimarisha
ustawi wa timu ya RUANGWA QUEENs na kuunga mkono jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu
kwa timu inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara.
Lengo la mchango ilikuwa ni kuipa hamasa timu ili ishiriki vyema katika ligi kuu Tanzania bara kwa
kuamini kuwa michezo ni ajira kwa vijana na fursa ya kuitangaza Ruangwa na mazuri yake
Tukio hilo liliwakutanisha viongozi wa timu, wawakilishi wa Ruangwa Queens Club, pamoja na
wafanyakazi wa kampuni yetu, na hivyo kuimarisha ushirikiano wa karibu kati ya taasisi na timu.
Hatua hii imeendelea kuonesha dhamira ya kampuni ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii
zinazolenga kujenga uhusiano chanya na wa kudumu na wadau wake.

Kampuni yetu inaendelea kujitolea kuchangia maendeleo ya jamii kwa vitendo, huku ikisisitiza maadili ya uwajibikaji, uaminifu, na huduma bora. Tunaendelea kuwaalika
wadau na wanajamii kushirikiana nasi katika safari ya kuleta mabadiliko chanya na yenye manufaa kwa jamii tunazohudumia.